Thursday 14 November 2013

NGUVU ZILETAZO MABADILIKO:



UNAWEZA KULETA MABADILIKO.
Yawezekana wakati mwingi  sasa umepita unahitaji mabadiliko katika ndoa yako,biashara yako,huduma yako,kazi yako,uhusiano wako na Mungu,au unakerwa na mambo katika familia yako,au katika taifa lako na umetafuta njia na misaada maeneo mbalimbali leo zimekufikia mkononi mwako,unahitaji kitabu kusoma kitabu hiki hakika hutakuwa kama ulivyokuwa na utasababisha na wengine kubadilika na kusababisha mabadiliko.
YALIYOMO KATIKA SOMO LETU.
Dhana Ya Mabadiliko

           Msukumo ulionyuma ya kutaka mabadiliko
Mifano ya watumishi waliowahi kuleta mabadiliko,
Aina mbalimbali za mabadiliko unayoweza kuyahitaji,
 Mambo Ya Kufanya Ili Kuleta Mabadiliko,
Mambo Ya Kufanya Ili Kuhakikisha Mabadiliko Yanatokea Na Yanadumu,
            Mabadiliko Katika Uchumi Wak,
Mabadiliko Katika Ndoa Yako,
 Mabadiliko Katika Eneo Lako La Kazi,
             Mabadiliko Katika Biashara Yako,
                    Mabadiliko Katika Uhusiano Wako Na Mungu,
Yeremia 18:7- 10.Wakati wowote nitakapotoa habari za taifa,na habari za ufalme,kuung’oa,kuuvunja,na kuuangamiza;ikiwa taifa lile nililolitaja litageuka ,na kuacha maovu yake,nitaghairi,nisitende mabaya yale niliyoazimia kuwatenda.Na wakati wowote nitakapotoa habari za taifa,na habari za ufalme,kuujenga na kuupanda,ikiwa watatenda maovu mbele za macho yangu,wasiitii sauti yangu,basi nitaghairi nisitende mema yale niliyoazimia kuwatendea.
Katika maisha tunayyoishi huku duniani kuna mambo unatamani kuyafanya lakini unajikuta unashindwa au unafanya lakini hayasogei na wakati mwingine unatumia nguvu kubwa na yanasogea kidogo
Mabadiliko ni sehemu ya maisha ya Mtu yeyote mwenye malengo hata yeye asiye na malengo,ni kawaida katika jamii Mtu kuzaliwa, kukua,kuoa,kuzaa kuzeeka na kufa ni mabadiliko ya kawaida ambayo Mtu huyapitia katika kukua
1.Nguvu ya toba katika kuleta mabadiliko.
2.Kufanya uamuzi sahihi ambao utakupeleka kufanyia kazi mipango unayotaka.
3.Having the altitude of change/shauku ya mabadiliko/ kiu ya mabadiliko/change of your mindset
4.Kufanya kwa bidii,uadilifu na ukamilifu/effectiveness and perfection in everything
5.Efective prayer towards the vision/Uombe kwa bidii} yaani juhudi na maarifa na kutokata tamaa mpaka umepokea.
6.Kuwa na maono/kusudi/malengo/kuunda vipao mbele.
7.Kujitoa mhanga with positive thoughts/ukubali kuangamiza nafsi au matamanio yako yasiyolenga kutimiza malengo yako.Yesu alisema kiungo kinachokusumbua kikate,heri ufike mbinguni kilema yaani  kuliko ukokosa kutimiza ndoto yako bora upunguze kwa nguvu baadhi ya matamanio yako kama vile marafiki,starehe,muda wa kupiga soga,vinywaji,eg.nilikuwa na rafiki mmoja aliamua kutumia boom la chuo kulipa ada ya mkewe kwa kuwa alikuwa na malengo Fulani yalyofungwa katika muda Fulani kwa hiyo alikuwa amepunguza milo,vinwaji na alikuwa akienda chuo kwa mguu na sio kwa gari kwa kuwa mabibo na chuo inawezekana kwa mguu kabisa kwa kuwa si mbali sana kiasi cha kuathiri muda wa masomo.
8.Ufahamu wa ki mungu kuhusu jambo unalotaka kulitenda ili ikujengee imani kwa mungu na kujua mungu yuko upande wako unapotenda jambo hilo.
9.Altitude Of excellence in every thing you do.
10.Uwe mwenye kutulia na kutafakari ili kuweza kugundua mambo ya kufanya na kubuni mbinu mpya za mafanikio katika eneo lako.yoshua 1:8,Isaya.   nguvu zenu zitakua katika kutulia na kutafakari
11.Ukubali kutotumia akili zako mwenyewe tu bali ukubali kuongozwa na Bwana. Mithali3:5 Wala usizitegemee akili zako mwenyewe,Isaya 48:17,55:8-12,zab 32:8,

No comments:

Post a Comment