Thursday 14 November 2013

USHAURI WA KIROHO

Founder of the Ministry
Ushauri wa kiroho kwa ajili yakoNamshukuru Mungu ambaye ametupa neema ya kukutana na wewe kwa njia ya maandishi ya kitabu hiki kinachohusu
maandalizi ya kumiliki malango ya adui. Siku zote maandalizi yanaonyesha nini kitatokea na kwa ukubwa kiasi gani. Mtu anayefanya maandalizi hafifu asitegemee kupata matokeo makubwa ya jambo analolilitegemea. Kwa upande mwingine mtu mwenye maandalizi makubwa na ya kutosheleza anatarajia
kupata matokeo makubwa katika jambo analolitegemea. Kumbe maandalizi ni sehemu ya muhimu zaidi kuliko kutenda jambo lenyewe, na maanadalizi siku zote huchukua mda mrefu zaidi kuliko mda ambao utatumika kwa tukio kutokea.Mara nyingi watu wengi huwa wanapigana na shetani bila
kufanya maandalizi ya kutosha, na hivyo wanajikuta kila mapambano yanapotokea wao ni wakushindwa tu. Sababu ni kwamba huna maandalizi ya kutosha ya kuweza kummilikiadui yako. Na wegine huwa wako katika mapambano ya mda mrefu katika jambo moja, maana yake ni kwamba huna mbinu za kiroho za kumiliki lango la adui katika hilo. Maandalizi ya kutosha yanaleta kumiliki lango la adui milele na kukusaidia wewe kuishi maisha ya ushindi siku zote Kitabu hiki kimeandaliwa mahususi kwa watu ambao wanataka kupigana vita vya kiroho kwa ufanisi na ushindi mkubwa kwa mda mfupi. Vita ya kiroho ipo kwa waliosimama vizuri na Beana Yesu, hivyo uwe umejiandaa au huna maandalizi yeyote lazima utapambana tu. Mara nyingi wengi wetu kwa sababu ya kutokuwa na maandalizi ya kutosha kabla ya vita huwa tunaishiwa nguvu katikati ya vita au kabla ya vita kuisha kwa sababu wakati unakwenda kupigana hukujua adui yako ana uwezo kiasi gani, anatumia silaha zipi, na mbinu gani. Ukisoma kitabu hiki na kufanya yote utaishi maisha ya ushindi.

No comments:

Post a Comment